Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza lilifungwa na mlinzi wa kati Nadir Haroub Ally 'Kanavaro' kulia.
Wengine kutoka kushoto ni Frank Domayo, Didier Kavumbagu na Simion Msuva.
|
Mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva akimtoka beki wa African Lyon Sunday Bakari kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.
|
Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea tena hii kwa
mchezo mmoja uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga
walikuwa wakiwakaribisha Afrikan Lyon.
Katika mchezo huo Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa
mabao 3-1.
Yanga ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza
lilizamishwa wavuni na mlinzi wa kati ambaye pia ni nahodha wa kikosi hicho, Nadir Haroub Ally ‘Kanavaro’ kabla ya
mshambuliaji Benedictor Mwamlangala wa Lyon kusawazisha katika kipindi
cha pili cha mchezo huo.
Aliyeizamisha Lyon hii leo alikuwa ni kiungo Nizar
Khalfani aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo akifunga mabao mawili ya dakika za 65 na 88 na kupelekea Yanga
kuchomoza na ushindi huo ambao umeifanya kufikisha jumla ya alama 7.
Yanga sasa inajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya mtani wake Simba mchezo ambao utachezwa Jumatano katika uwanja wa Taifa.
Tayari maandalizi ya mchezo huo yamekwisha aanza kwa kila upande huku Simba ikiwa imejichimbia huko Zanzibar wao Yanga wako kambini huko Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment