KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, September 25, 2012

KILA LA KHERI SERENGETI BOYZ KAMA MAANDALIZI YAMEWAINGIA KWELI KWELI SASA NYONGA MISRI IDADI KUBWA YA MABAO.

Serengeti Boys chini ya Kocha Jakob Michelsen na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ikiwa na wachezaji 28 iko kambini jijini Dar es Salaam tangu Agosti 27 kujiandaa na mchezo wa hatua ya pili kuwania kucheza fainali za mataifa ya Afrika ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya Misri.
 Serengeti Boys chini ya Kocha Jakob Michelsen na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo maarufu 'Julio' iko kambini na jumla ya wachezaji 28 tangu Agosti 27 ikijiandaa na mchezo wake wa kwanza wa mzunguko wa pili dhidi ya Misri utakaochezwa Oktoba 12.
Wachezaji waliko kambini ni makipa Abdallah Bakar (Mjini Magharibi), Hamad Juma (Azam) na Peter Manyika (JKT Ruvu). Mabeki ni Abdallah Salum (Mjini Magharibi), Basil Seif (Morogoro), Hassan Mganga (Morogoro), Ismail Gambo (Azam), Mgaya Abdul (Azam), Miraji Selemani (Polisi Morogoro), Miza Abdallah (Kinondoni), Mohamed Hussein (Azam), Pascal Matagi (Dodoma) na Paul James (Kinondoni).
Viungo ni Farid Musa (Kilimanjaro), Hussein Twaha (Coastal Union), James Mganda (Kipingu Academy), Mbwana Ilyasa (Simba), Mohamed Haroub (Zanzibar), Mohamed Kapeta (Kinondoni), Mudathiri Yahya (Azam), Mzamiru Said (Morogoro) na Selemani Bofu (JKT Ruvu).
Washambuliaji ni Abdallah Kisimba (Mwanza), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda (Mwanza), Joseph Lubasha (Azam), Kelvin Friday (Azam) na Salvatory Nkulula (Kipindu Academy).
Mechi ya kwanza itachezwa nyumbani kati ya Oktoba 14 mwaka huu wakati ambapo mechi ya marudiano ikitarajiwa kuchezwa kati ya Oktoba 26, 27 na 28 mwaka huu.
Misri ni kati ya timu 17 zilizoingia moja kwa moja raundi ya pili kama ilivyo kwa Serengeti ambayo ilipita round ya kwanza kufuatia timu ya Kenya kujitoa.
Timu nyingine ni Afrika Kusini, Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Congo Brazzaville, Cote d’Ivoire, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Mali, Rwanda, Senegal, Sierra Leone, Tunisia na Zambia.
Kwa namna ambavyo Serengeti imekuwa ikijifua tangu wakati huo mpaka sasa, imeanza kupewa matumaini makubwa hasa kufuatia matokeo ya michezo yake iliyofanyika kuanzia Dar es Salaam mpaka kule Mbeya ambako ilikuwa imeweka kambi kwa takribani wiki nzima.
kocha msaidizi wa timu hiyo Jamhuri Kihwelu maarufu kama Julio amekuwa akisifia nidhamu kimchezo mpaka tabia za wachezaji wake ndani na nje ya uwanja.
amesema sasa timu hiyo inaweza kucheza na timu yoyote ile kwa kuwa wachezaji wako sawa sawa kiakili, kimazoezi na kisaikolojia hivyo hana shaka na kikosi.
Rockersports imekuwa karibu na vijana hao na imekuwa ikifuatilia maandalizi yao kuanzia ndani ya kambi mpaka nje kujua maisha ya wachezaji hao vijana wanavyo jengwa kisoka ili kulitoa aibu Taifa hili la Tanzania.
Kila la kheri Serengeri Boys.

No comments:

Post a Comment