Aliyekuwa kocha mkuu wa Coast Union ya Tanga Jauma Mgunda ameamua kumwaga manyanga ya kuifundisha timu hiyo kutokana na sababu ambazo hazija fahamika huku uongozi wa Coast Union ukithibitisha taarifa za kocha wao huyo kujiondoa katika benchi la ufundi.
Akiongea na Rockesports Mgunda amesema ameamua kujiweka pembeni kwa kuwa ameona muda umefika kwa yeye kuachia nafasi hiyo na kuendelea na mambo mengine.
Mgunda amesema lengo lingine ni kuacha nafasi ya kwa malengo makubwa ya Coast kutimia kwa kuwa klabu hiyo imekuwa na malengo makubwa.
Kwa upande wake kiongozi mkuu wa timu hiyo Hemed Aurora amesema amepokea maamuzi ya Mgunda bila kufafanua kwa uwazi nini sababu za kocha huyo kuachia ngazi.
Mgunda ameondoka katika benchi la ufundi la timu hiyo ikiwa na points tano baada ya michezo mitatu ya ligi kuu Tanzania Bara.
Timu hiyo sasa itakuwa chini ya Juma Pondamali 'Mensa' na Razack Yusufu 'Kareka'
Timu hiyo sasa itakuwa chini ya Juma Pondamali 'Mensa' na Razack Yusufu 'Kareka'
Bofya hapa chini
No comments:
Post a Comment