KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 26, 2012

SIMBA KUMKOSA EMMANUEL OKWI MECHI YAO NA MTANI YANGA OCTOBA 3

Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba 25 mwaka huu) kupitia ripoti za mechi 21 za Ligi Kuu ya Vodacom ambazo zimeshachezwa mpaka sasa, na kuzifanyia uamuzi wa kikanuni ikiwemo kumuondoa Kamishna mmoja

Pamoja na mambo mengine kamati hiyo imethibitisha kadi nyekundu ya Emmanuel Okwi kwa kumpiga kiwiko Kessy Mapande wa JKT Ruvu, hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(1)() anakosa mechi tatu na kulipa faini ya sh. 500,000. Mchezaji huyo atakosa mechi namba 20, 27 na 80.

Mchezo namba 20 ni dhidi ya Ruvu Shooting ambao ameshatumikia adhabu nyake, mchezo na 27 ni dhidi ya Tanzania Prisons ambao utachezwa tarehe 27/09/2012 na mchezo namba 80 ni dhidi ya mtani wake Yanga ambao utachezwa octoba 3 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Kwa upande wa waamuzi, Ronald Swai ameandikiwa barua ya onyo kutokana na upungufu alioonesha kwenye mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
George Komba aliyekuwa Kamishna kwenye mechi namba 20 kati ya Simba na Ruvu Shooting ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi kutokana na upungufu uliojitokeza katika ripoti yake.
 
Mambo mengine yaliyopitiwa na kutolewa maamuzi ni pamoja na klabu kuandikwa barua za onyo ambazo ni African Lyon kwa kwenda uwanjani na jezi tofauti na zile ilizoonesha kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (pre match meeting), Mtibwa Sugar kwa kuchelewa kuwasilisha leseni za wachezaji wake wakati wa mechi na Ruvu Shooting kwa ushangiliaji uliopita kiasi kwenye mechi yao dhidi ya Simba.
 
Wamiliki wa viwanja vya Mkwakwani, Tanga na Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya wameandikiwa barua ya kuvifanyia marekebisho viwanja vyao katika maeneo mbalimbali yenye upungufu ikiwemo uzio wa kutenganisha wachezaji na washabiki.
 
Mchezaji Faustin Lukoo wa Polisi Moro ambaye kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi aliyemtoa nje kwa kadi nyekundu alimtukana mchezaji mwenzake kwenye mechi dhidi ya African Lyon na Katibu wa Oljoro JKT aliyemwaga maji kwenye chumba cha timu ya Polisi Moro, masuala yao ni ya kinidhamu, hivyo yamepelekwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi kwa ajili ya hatua zaidi.
 
Kwa klabu ambazo timu zao mpaka sasa zinacheza mechi bila kuwa na logo ya mdhamini, suala hilo limepelekwa kwa wadhamini Vodacom kwa vile wenyewe ndiyo wanaogawa vifaa hivyo.

No comments:

Post a Comment