KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 17, 2012

NGUMI ZA RIDHAA TAIFA ZAANZA HII LEO UWANJA WA NDANI WA TAIFA.


Michuano ya ngumi za ridhaa ya Taifa imeanza hii leo katika uwanja wa wa ndani wa Taifa ambapo jumla ya mikoa 18 imetuma wachezaji wake kushiriki michuano hiyo.

Mchezo hiyo itashirikisha ngumi za uzito mbalimbali ambapo hii leo Saidi Hofu wa JKT amefanikiwa kumchapa Emmanuel Mogela wa Ilala ukiwa ni mchezo wa kwanza ambapo pia Joseph Master wa Arusha alifanikiwa kumchapa Fadhili Hassan wa Pwani kwa Points.

Michezo imepangwa kuchezwa round tatu kila pambano ambapo washindi watakuwa wakivuka kuingia katika hatua ya robo fainali, kabla ya hatua ya nusu fainali na kumalizia hatua ya fainali.

Akiongea na Rockersports katibu wa chama cha ngumi za Ridhaa nchini Makore Mashaga amesema ufunguzi rasmi wa michezo hiyo itakuwa ni hapo kesho.

kwa mujibu wa ratiba michezo hiyo itakuwa ikianza mapema asubuhi na kuendelea mpaka jioni ambapo amewata wakaazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuwashangilia wachezaji kutoka mikoa yao walikotoka kwa kuwa Jiji la Dar es Salaam lina mkusanyiko wa watu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment