SHIRIKISHO la Soka
Tanzania (TFF) limesema litazikata baadhi ya klabu sehemu ya fedha
zitakazotolewa na wadhamini wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara (Vodacom), ili
kufidia deni linalozidai klabu hizo.
Akizungumza na waandhishi wa habari hii leo, Rais wa TFF Leodegar Tenga amesema hatua hiyo ina lengo la kufidia madeni yao baada ya klabu hizo kutolipa kwa muda mrefu.
Tenga amebainisha madeni hayo kufuatia kujitokeza kwa baadhi ya vilabu ambavyo vimejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kusema kuwa vinaidai TFF fedha zilizotolewa na na
wadhamini hao kwenye msimu wa 2011.
"Ni kweli kuwa
kuna klabu chache ambazo zinadai malipo ya fedha kutoka kwa wadhamini za msimu
uliopita, lakini TFF kama baba na klabu ni watoto. Hivyo nasi kuna klabu kadhaa ambazo tunazidai, nasi
tutazikata kutoka kwenye fedha za wadhamini zinzotarajiwa kupatikana hivi
karibuni," alisema.
Tenga amesema kinachofanyika kwa sasa ni kuwapa kazi wakaguzi wa mahesabu, ambao amesema watapitia madeni ya vitabu na mahesabu kufanyika ili
kubaini ni klabu gani na kiasi gani kinachodaiwa.
Amesema klabu hizo
zililipiwa madeni kwenye Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kufanya makosa na kutatakiwa kulipa faini.
Wakati huo huo, Tenga
ametoa wito kwa wadau na wamiliki wa makampuni na taasisi za fedha, kujitokeza
kwa wingi na kuzidhamini timu za taifa za vijana na ile ya wanawake (Twiga Stars).
Amesema kwa kufanya
hivyo ni wazi kutaziwezesha timu hizo kuwa na uwezo wa kufanya maandalizi
mazuri na ya muda mrefu kabla ya kukabiliana na ushiriki kwenye michuano ya
kimataifa.
Katika hatua nyingine Tenga
amezitaka klabu ambazo mechi zake zitaonyeshwa na kituo cha televisheni cha
Super Sports cha Afrika Kusini, kuonyesha soka safi ili kulitangaza vema soka la Tanzania.
No comments:
Post a Comment