Song: Ilikuwa ngumu kukataa kujiunga na Barcelona
Kiungo Alex Song amesisitiza
kuwa ilikuwa kwake ngumu kukataa kujiunga na Barcelona baada ya timu hiyo kigogo
nchini Hispania kuonyesha nia ya kumtaka.
Kiungo huyo mwenye
nguvu, uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na mwepesi kuamua,
alijiunga na ‘Blaugrana’
akitokea Arsenal katika kipindi cha uhamisho wa kiangazi kilichopita.
Amenukuliwa na
El Mundo Deportivo akisema
"Kama Barca
wanakutaka inakuwa ngumu kusema hapana. Nafasi kama hiyo inatokea mara
moja katika maisha na hutakiwi kuikosa"
"mara
ya kwanza kufahamu kuwa wananitaka ilikuwa July. Waliongea na Arsenal, na Arsene
Wenger akanifuata na kuniambia. Ilikuwa ngumu kumshawishi Wenger na kumpa mkono
wa kwaheri, kwasababu alinisaidia mimi na familia yangu mambo mengi nilipofika nikiwa na umri wa miaka 17."
Kwasasa m-Cameroon
huyo anasuburi kwa hamu kubwa mchezo mgumu na wa historia katika soka la Hispania,
El Clasico, na anasisitiza kuwa atakuwa zaidi ya tayari kucheza endapo meneja
wake atamchagua.
Amenukuliwa
akisema
"sijui
kama nitapangwa dhidi ya Real Madrid. Ni juu ya Tito Vilanova, ni wazi kuwa
tutakuwa na nguvu mimi, Carles Puyol pamoja
na Gerard Pique, lakini niko tayari kwa kazi. Nimecheza dhidi ya Cristiano
Ronaldo kabla ya kuja hapa nikiwa katika Premier League."
Barcelona itakuwa
wenyeji wa Real Madrid Oct. 7, lakini kabla ya mchezo huo itakuwa kwanza na
michezo miwili dhidi ya Sevilla na Benfica.
Real Madrid yaomboleza kifo cha
mchezaji kinda
Real Madrid inaomboleza
kifo cha mchezaji wao mototo Benjamin Alonso Ezquerra, ambaye amefariki dunia
baada ya kugongwa na gari jumatatu iliyopita.
Kwa mujibu
wa jarida la AS, Ezquerra, ambaye alijisajili na kikosi cha watoto ambacho
ni sehemu ya mpango wa maendeleo wa muda mrefu wa klabu hiyo june 11, aligongwa
wakati akivuka katika mtaa wenye msongamano mkubwa akitatafuta mpira uliopotea.
Taarifa ya
Madrid imeonyesha kusikitishwa na kuhuzunishwa na msiba huo wa ghafla.
Imenukuliwa taarifa
hiyo ikisomeka
"Real
Madrid CF imesikitishwa na imehuzunishwa sana na kifo cha mchezaji Alonso
Ezquerra, na inaungana na familia yake na marafiki zake katika kipindi hiki
kigumu."
Alvaro
Morata, kiungo mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni hivi karibuni amejiunga na
timu hiyo naye ametuma salamu zake za maombolezo kwa familia ya Ezquerra kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
umenukuliwa ujumbe
wake ukisomeka klabu nzima ni familia ya Ezquerra".
"wote
tunaungana kuelekea katika familia yake. Rest in peace."
Kiungo wa Real Madrid Ozil akanusha kuwa anajichanganya mno
Nyota wa Real
Madrid Mesut Ozil ameendelea kukanusha taarifa kuwa, amekuwa mtu wa
kujichanganya sana nyakati za usiku na hivyo kuathiri kiwango chake uwanjani.
Meneja Jose
Mourinho amekuwa akihusishwa na tabia ya kijana wake huyo mwenye umri wa miaka
23 nje ya uwanja na ntaarifa zaidi zikiarifu kuwa tabia ya kujichanganya sana
kwa Ozil kumeshusha kiwango chake katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Hata hivyo
kiungo mshambuliaji huyo hii leo ameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa
kijamii wa facebook kuwa anazipuuza taarifa hizo na kusisitiza kuwa hakuwa
ukweli wowote juu ya hilo.
Amenukuliwa akisema
"juu ya
tetesi kuwa nakwenda sana nje usiku, si kweli. Na tangu nianze msimu sijawahi kutoka
usiku. Nafanya mazoezi kama mchezaji professional," .
No comments:
Post a Comment