Vodacom yazungumzia kipengele cha Upekee (Exclusivity) katika mkataba wa udhamini
wa Ligi Kuu.
Dar es salaam 25th
September 25, 2012, Kampuni ya
Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imesema suala la kuwepo kwa kipengele cha Upekee “EXCLUSIVITY”
katika mkataba wa udhamini wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya kampuni hiyo
na shirikisho la soka nchini - TFF ni la muhimu katika kuepuka migongano ya
kimasilahi ya kibiashara miongoni mwa wadhamini.
Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom Tanzania Bw Kelvin
Twissa amesema kampuni ya Vodacom inajali na kuthamini maendeleo ya vilabu
nchini na kwamba itaendelea kufanya hivyo kwa kutoa fursa zaidi zinazolenga
kukuza kiwango cha uwekezaji katika soka kwa masilahi ya vilabu na taifa kwa ujumla.
Twissa amesema katika kutambua umuhimu wa kupanua wigo wa uwekezazi katika
ligi kuu ya Vodacom na maendeleo ya vilabu kwa ujumla, kampuni ya Vodacom Tanzania
ilikubali kwa moyo mkunjufu kuruhusu vilabu kutafuta wadhamini wengine ambao siyo
makampuni yanayofanya baishara sawa na Vodacom.
Twissa alikuwa akizungumza katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha
Shirikisho la Soka Tanzania – TFF, Kamati ya Ligi Kuu na Mdhamini Mkuu kampuni
ya Vodacom Tanzania kilichoketi jana
jijini Dar es salaam.
“Tunatambua na kuheshimu utayari wa makampuni mengine ambayo yapo tayari
kushirikiana na sisi katika kudhamini Ligi kuu ya Vodacom nasi tupo tayari
kushirikiana nao na hivyo kuleta maendeleo ya mpira wa miguu nchini”Alisema
Twissa
“Vodacom Tanzania inajivunia kuwa wadhamini wakuu wa ligi hii,tumeamua
kuboresha udhamini wetu kwa sababu tunatambua umuhimu wa michezo kwa Taifa
letu, sasa michezo si kwa ajili ya burudani tu bali imekuwa chanzo cha ajira na
kuboresha maisha ya wanaojihusisha nayo,” Aliongeza Twissa.
“Tunaviomba vilabu vinavyoshiriki
ligi kuu, vyombo vya habari na umma kwa ujumla kutambua kuwa azma ya Vodacom ni
kuona mpira wa miguu unasonga mbele zaidi na ndio maana tumekuwa katika udhamni
huu kwa zaidi ya miaka saba tukipitia vipindi tofauti lakini hatukuwahi kukata
tamaa. Hivyo si vyema wakati huu soka yetu inapokua tukaruhusu hali inayoweza
kusababisha changamoto katika uwekezaji wa soka.” Aliongeza Twisa
Twissa amesema kampuni ya Vodacom itaendelea kushirikiana na TFF, Kamati ya
Ligi na wadau wengine wote wa mpira wa miguu nchini katika kukuza uwekezaji kwa
kusaidia vilabu kupata wadhamini watakaosaidia maendeleo ya vilabu hivyo.
Mwisho.
Taarifa hii imekuja ikiwa ni kujibu matakwa ya vilabu vya ligi kuu kuondolewa kipengele hicho cha UPEKEE" EXCLUSIVITY"ambacho kimsingi kinakataza vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo kuvaa nembo yoyote ya kibishara ambayo inafanana kampuni ya kibiashara inayotoa huduma ya simu za mikononi.
Klabu ya Afrikan Lyon hivi karibuni ilipata udhamini toka kambuni nyingine inayotoa huduma ya simu za mikononi ya Zantel udhamini ambao ulileta tafrini kubwa hasa pale timu hiyo ilipotaka kuvaa jezi zilizo kuwa na nembo ya mdhamini wao huyo katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu Septemba 15 dhidi ya Simba.
Mbali na kutaka kuvaa lezi hizo, pia walitaka kuweka mabango yenye nembo nembo ya Zantel uwanjani jambo ambalo lilipingwa vikali na shirikisho la soka TFF na kusababisha gumzo ambalo lilipelekea kikao cha pamoja cha wadau hao wakuu.
No comments:
Post a Comment