KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, December 19, 2012

IKULU YAPOKEA MAKOMBE MBALIMBALI YA SHIMIWI NA KUPONGEZA WANAMICHEZO WAKE. HAFLA ILIFANYIKA JUZI JUMATATU.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipozi na kikosi kizima cha wanamichezo mbalimbali wa Ikulu Sports Club ambacho kilinyakua jumla ya makombe matano katika michezo mbalimbali ya Shirikisho la Michezo ya Wizara  (SHIMIWI)  mwaka huu mjini Morogoro. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Ikulu Bw Julius Mogore katika hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora  iliyofanyika leo Deswemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwakq huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara  56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya Baiskeli, Netbal,  Kuvuta kamba wanawake na wanaume  na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akinyanyua juu mojawapo ya makombe matano ambayo Ikulu Sports Club ilinyakua kwenye michezo ya SHIMIWI ya  maka huu mjini Dodoma katika  hafla ya kukabidhi makombe na kuwazawadia wafanyakazi bora iliyofanyika leo Desemba 17, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam. Kwenye michezo hiyo iliyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 10 mwakq huu, ilishirikisha jumla ya wanamichezo 3500 kutoka wizara  56, mikoa 18 na idara za serikali 14 ambapo wanamichezo 91 wa Ikulu walioshiriki walifanikiwa kuibuka washindi wa kwanza katika michezo ya Baiskeli, Netbal,  Kuvuta kamba wanawake na wanaume  na kushik nafasi ya pili ya riadha kwa wanawake na wanaume.

No comments:

Post a Comment