KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 29, 2013

RAIS OBAMA NI KAMA RAIS KIKWETE, RAIS WA WATU KATIKA NCHI YA WATU. AKUTANA NA WACHEZAJI WA MIAMI HEAT IKULU KTK HAFLA YA USHINDI WA TAJI LA NBA.


  Kama ilivyo kwa Rais Kikwete ambaye mara kadhaa amekuwa akipenda kuwalika ikulu wanamichezo na wasanii wa fani mbalimbali kwa lengo la ama kuwapongeza au kuwasikiliza panapo tokea mambo mbalimbali ambayo yanahitaji busara zake, ndivyo ilivyo kwa Rais wa Marekani Barak Obama.

LeBron James na wachezaji wenzake wa Miami Heat hii leo wamefika ikulu ya marekani maarufu kama White House ikiwa ni sehemu ya sherehe zao za kufanikiwa kutwaa taji la ligi ya mpira wa kikapu waliloshinda msimu uliopita.

Miami Heat waliibuka mabingwa wa taji hilo baada ya kuwafunga Oklahoma City Thunder mara nne huku na Thunder kushinda mara moja na kutwaa taji hilo.

Mchezaji anayependwa na mashabiki wengi wa mpira wa kikapu ambaye ni pia ni miongoni mwa watu maarufu nchini Marekani LeBron James ambaye pia alishinda tuzo ya mchezaji bora MVP baada ya michuano hiyo, alikuwa kinara katika hafala hiyo.
The Miami Heat won the NBA Finals last year
Miami Heat waliibuka mabingwa wa NBA mwaka 2012.
LeBron James mwenye miwani mchezaji bora wa NBA baada ya kushinda series dhidi ya Thunder.
 Baadhi ya wachezaji akiwemo James mwenyewe waliwahi kupata nafasi ya kucheza kikapu na Rais Obama katika hafla ya Rais huyo kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwake mwaka 2010.
Obama ambaye ni shabiki wa Chicago Bulls, alikuwa na wakati mzuri wa kutaniana na wachezaji hao wakati wa tukio hilo akisema 
 'Sasa sistahili kuchukua sifa zote za ukocha lakini nadhani iko wazi wanaostahili ni Kevin Durant na Russell Westbrook.
 The basketball star seemed slightly nervous at the event
LeBron akimkabidhi Rais Obama mpira uliosainiwa na wachezaji wote wa Miami Heat.
The Heat overcame the Oklahoma City Thunder in the Finals
 Rais Obama kwa dhati kabisa aliwapongeza Miami Heat kwa kutwaa taji hilo.
 alikaririwa akisema
'Hii timu imesafiri safari ndefu mpaka kufikia hapo' 

Hapo alikuwa akilinganisha na mwaka 2011 ambapo walifikia hatua ya fainali lakini wakapoteza kwa Dallas Mavericks.
Aliendelea kusema,
'Unapodondoka, mtihani kwako ni kusahau yaliyopita na kuwadharau wanaowabeza, unachopaswa kufanya ni kuinuka tena na kurudia kwa nguvu, huo ndio ukweli katika Basketball, lakini ndio ukweli katika maisha.'

Pia amewapongeza wachezaji wote kwa kujituma na kuwa mfano kwa vijana anao inukia katika mchezo huo ambapo wengi wao wamekuwa wakiwatazama kama role models nchi Marekani.
Kwa upande wake LeBron kwa niaba ya wenzake amesema wamefurahishwa kupata si ya kumtembelea Rais Ikulu ya  Washington DC.
Amenukuliwa akiuliza,
 'Naweza kusema kitu?' halafu kwa unyenyevu mkubwa akaelekea kwa Rais na kumkabidhi mpira ulitiwa saini na wachezaji wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment