Ndivyo ambavyo Lampard alivyopiga mpira uliozaa goli la pili na kumpita Julio Cesar.
Tazama mpira wa Lampard uliozaa goli safi la pili.
|
Bao safi la Frank Lampard katika kipindi cha pili limeiwezesha England kupata ushindi dhidi ya vijana wa Samba Brazil katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika dimba la Wembley.
Ushindi huo umekuwa ni mwendelezo wa sherehe za maadhimisho ya miaka 150 kuanzishwa kwa chama cha soka cha England FA ambapo England pia rekodi ya kuifunga Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la dunia.
Wayne Rooney ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunga bao uongozi kipindi cha kwanza muda mfupi baada ya penati ya Ronaldinho kuokolewa kistadi na mlinda mlango Joe Hart. Fred aliyeingia kipindi cha pili alifanikiwa kuisawazishia Brazil bao lakini Frank Lampard aliyeingia kipindi cha pili kuandika bao la pili kwa shuti ambalo liligonga mwamba wa kushoto wa mlinda mlango Julio Cesar na kutinga wavuni.
Hata hivyo kikosi cha kilicho katika nafasi ya 6 katika viwango vya ubora vya FIFA kilionekana kikitawala mchezo kwa sehemu kubwa ukilinganisha na Brazil ambao katika viwango vya ubora vya FIFA wako katika nafasi ya 18 huku kiungo Jack Wilshere akitawala vema sehemu ya kiungo.
Uwanja wa Wembley
ulikuwa ukisubiri kwa hamu ujio wa nyota wawili wa Brazil Neymar na Ronaldinho, lakini wote walionekana kutokuwa vizuri licha ya kuwa ndio kioo cha Brazil kabla ya mchezo
Frank Lampard akikimbia kwa furaha baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Brazil.
Ndivyo ambavyo Lampard alivyopiga mpira uliozaa goli la pili na kumpita Julio Cesar.
Tazama mpira wa Lampard uliozaa goli safi la pili.
Wayne Rooney akiruka juu akishangilia goli la kwanza dhidi ya Brazil uwanja wa Wembley.
Julio Cesar akizuia mpira wa Theo Walcott akiwa karibu na goli baada ya kupokea pasi ya Jack Wilshere.
Fred wa Brazil akifunga goli la kusawazisha kipindi cha pili kufuatia makosa ya Gary Cahill.
David Luiz akiongoza furaha ya goli la kusawazisha lililofungwa na Fred.
...Ronaldinho kipiga penati ambayo haikuzaa goli..
Ronaldinho akitahidi kupiga mpira kuelekea katika lango la England lakini Joe Hart alikuwa imara.
Neymar akitengeneza mpira huku akikabiliwa na upinzani kutoka kwa Tom Cleverley.
Peter Shilton akimkabidhi nahodha wa England Steven
Gerrard kofia ya kumbukumbu ya dhahabu ikiwa ni ishara ya heshima kwake baada ya kutimiza michezo 100 ya kuitumikia England mwezi Novemba katika mchezo dhidi ya Sweden mwaka jana.
Sanamu ya nyota na nahodha wa zamani wa England Bobby Moore iliyowekwa nje ya uwanja wa England ilikuwa ni kumbukumbu yake ya miaka 20 tangu kufariki dunia wiki hii.
Akina dada wakicheza Samba kuwafurahisha watazamaji zaidi ya elfu 80 waliohudhuria mchezo huo ikiwa ni ngoma maarufu Marekani ya kusini.
Mshabiki wa Brazil.
Wacheza shoo wakionyesha shoo ya ngoma ya kibrazil ndani ya uwanja wa Wembley.
Ronaldinho akipewa jezi ikiwa ni ishara ya utumishi wake wa michezo 100 katika kikosi cha Brazil jezi hiyo imechorwa namba 100.
Luiz Felipe Scolari ameiongoza Brazil dhidi ya England akirejea baada ya kupigwa chini mwaka 2006.
No comments:
Post a Comment