Nigeria imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Afrika kwa mwaka 2013 baada ya kuibanjua Mali kwa mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Moses Mabhida jumatano usiku.
Nigeria iliandika bao la uongozi katika dakika ya 25 kwa kichwa cha kuchumpa na mlinzi Elderson Echiejile ndani ya sanduku la hatari na kumpita mlinda mlango Victor Moses upande wake wa kulia.
Waliongeza bao la pili katika dakika ya 30 lililofungwa na Brown Ideye akimalizia krosi ya Emmanuel Emenike.
Emenike mwenyewe aliandika bao lake la 3 dakika moja kabla ya mapumziko kufuatiam mpira aliopiga akiwa nje ya kisanduku cha hatari kupoteza mwelekeo na kumpita mlinda mlango wa Mali Mamadou Samassa nyuma.
Badilko lililofanywa na Nigeria la kumuingiza Ahmed Musaab lilizaa matunda baada ya kuiandikia Nigeria bao la 4 kunako dakika ya 60.
Mali iliandika bal akufuatia machozi kunako dakika 75 kupitia kwa Cheick Diarra baada ulinzi wa Nigeria kupoteza umakini.
No comments:
Post a Comment