KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 9, 2013

LIGI DARAJA LA KWANZA TESSEMA NA VILLA SQUAD HAPATOSHI MLANDIZI KESHO ASHANT NA TRANSCAMP KARUME SHUGHULI NYINGINE HIYO KUSAKA TIKETI YA KUPANDA LIGI KUU.

Kikosi cha Ashant kinakazi kesho dhidi ya Transcamp uwanja wa Karume.
 Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuwania tiketi za kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao inaendelea kutimua vumbi wikiendi hii kwa mechi kumi na moja zitakazopigwa kwenye viwanja mbalimbali.

Kundi A kesho (Februari 10 mwaka huu) Mbeya City itacheza na Polisi Iringa katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Mkamba Rangers itaumana na Burkina Faso (Uwanja wa CCM Mkamba) wakati JKT Mlale itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Green Warriors na Ndanda zinacheza hii leo (Februari 9) kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B. Mechi nyingine kundi hilo leo ni kati ya Tessema na Villa Squad kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Kesho(Februari 10)Transit Camp itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam wakati Polisi Dar es Salaam na Moro United zitavaana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.

Kundi C kesho (Februari 9 mwaka huu) ni Polisi Dodoma vs Polisi Tabora (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Polisi Mara vs Mwadui (Uwanja wa Karume, Musoma), Morani vs Kanembwa JKT (Uwanja wa Kiteto, Manyara) na Rhino Rangers vs Pamba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

No comments:

Post a Comment