KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 9, 2013

AZAM YAELEKEA MANUNGU LEO KUIVAA MTIBWA KESHO IKIWA NA KIKOSI KAMILI.

Timu ya soka ya Azam FC imesafiri leo kuelekea Manungu Turiani mkoani Morogoro kukwaana na Mtibwa Sugar mchezo ambao utafanyika kesho


Azam FC imesafiri na kikosi chake chote cha wachezaji 25 na viongozi nane ambao ni Dr Twalib, Gomes, Kally Ongala, Jemedary Said, Iddi Abubakar, Ibrahim Shikanda na Stewart Hall

Wachezaji wa kigeni waliokuwa na majukumu katika timu za taifa, Humphrey Ochieng Mieno na Jockins Atudo walirejea jana usiku huku Brian Umony akiwasili hapo mchana jana.

Leo asubuhi kabla ya safari Azam FC ilifanya mazoezi kwenye kambi yake iliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam

Azam FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 30 nyuma ya Yanga yenye pointi 33 na Simba ikishika nafasi ya tatu ikiwa n pointi 27.
Endapo Azam itafanikiwa kushinda mchezo wake wa kesho dhidi ya Mtibwa sugar basi itakuwa imefikisha alama sawa na Yanga ambayo inaongoza katika msimamo ligi kuu ya soka Tanzania Bara ikiwa na alama 33 na Azam fc ikiwa na alama 30, Yanga ikiwa na uwiano mzuri wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ukilinganisha na Azam.

Yanga imefunga magoli 29 na kufungwa 12 ilhali Azam ikiwa imefunga magoli 23 lakini pia imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara 13, hivyo mazingira yanaonyesha bado Yanga itakuwa na nafasi kubwa ya kuendelea kuongoza ligi hiyo vinginevyo Azam ishinde zaidi ya magoli 6 na isiruhusu nyavu zake kutikiswa dhidi ya Mtibwa sugar hiyo kesho. 
Kikosi cha mtibwa Sugar.
Wao Mtibwa Sugar mara baada ya kwenda sare na Yanga katika mchezo uliopita, watakuwa wakihitaji ushindi wakiwa katika dimba la nyumbani Manungu Turiani dhidi ya Azam fc na kukusanya alama 3 muhimu ambazo zitawafanya kufikisha alama 26 sawa na Coast union iliyo katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment