KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 9, 2013

VAN NISTERLROOY; MANCHESTER UNITED DHIDI YA REAL MADRID JUMATANO NI RONALDO DHIDI YA VAN PERSIE

Star man: Cristiano Ronaldo
Deadly: Robin van Persie

Ruud van Nistelrooy anaamini viwango vya sasa vya wachezaji Robin van Persie na Cristiano Ronaldo vitakuwa ndio chachu ya maamuzi ya ushindi wa mchezo wa hatua ya mtoano wa 16 bora wa vilabu bingwa barani Ulaya baina ya vilabu vyake vya zamani vya Manchester United na Real Madrid.
Van Nistelrooyano aliitumikia United kwa miaka mitano kabla ya kuelekea Madrid mwaka 2006 ambako aliitumikia kwa miaka minne katika viunga vya Bernabeu, anadhani kuwa ni vigumu kujua ni timu gani kali kati ya hizo mbili itakayo ibuka na ushindi. 
Ruud van Nistelrooy anaadhani mpiga mabao wa United, Van Persie na mpiga mabao wa Madrid ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa United, Ronaldo ndio wa kura ya timu gani itaibuka na ushindi jumatano.
Amenukuliwa na gazeti la Marca akisema,
 'kwa upande wangu utofauti utaletwa na viwango vya uchezaji vya Cristiano na Van Persie. Nadhani mmoja kati ya wachezaji hao ataleta utofauti wa matokeo ya mchezo,' 
'Timu zote zinafanya vizuri. Nadhani Madrid imeimarika kwa kiasi kikubwa katika wiki za hivi karibuni, achilia mbali matokeo ya mchezo dhidi ya Granada ambapo walifungwa goli 1-0. Naiona ni timu ngumu, ambayo ilicheza vizuri dhidi ya Barca na wanaonyesha ubora wao katika michezo migumu.
'Nadhani mtanange huo utaamuliwa na vitu vidogo.'
Split loyalty? Ruud van Nistelrooy left Manchester United for Real Madrid in 2006
Split loyalty? Ruud van Nistelrooy left Manchester United for Real Madrid in 2006  

Ruud van Nistelrooy aliihama Manchester United na kujiunga na Real Madrid mwaka 2006.

What about me? Wayne Rooney, who scored for England this week, has found a run of form
Wayne Rooney, ambaye alifunga goli la England wiki hii amerejea katika kasi yake.

Mduchi Ruud van Nistelrooy mwenye umri wa miaka 36 anadhani Madrid ambayo inasaka rekodi ya kushinda taji la Ulaya kwa mara ya 10 imeimarika zaidi kiubora kuliko kikosi cha Sir Alex Ferguson lakini ameionya Madrid kuwa makini na uwezo wa safu ya ushambuliaji ya United ambayo ina washambuliaji wenye uchu wa magoli kama Van Persie na Wayne Rooney.
'Madrid kutokana na kukabiliwa na majeruhi haijaweza kuunga kikosi imara na kupata kikosi kimoja kilicho imara kila wiki.
 'Pepe na Marcelo wamekuwa majeruhi, Gonzalo Higuain na Karim Benzema hawako vizuri, Angel  Di Maria hachezi mara kwa mara, pamoja na majeruhi kwa mlinda mlango Iker Casillas.
Clinical: Ronaldo has an incredible scoring record for Real Madrid, who he joined for £82million from Manchester United
Ronaldo amekuwa mfungaji wa Real Madrid tangu ajiunge nayo kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 82 akitokea Manchester United.
The difference: Both Sir Alex Ferguson and Roberto Mancini believe the addition of Van Persie has propelled United to the top
Sir Alex Ferguson na Roberto Mancini wanaamini Van Persie amekuwa jembe la kuipeleka United kileleni.
Returning hero: Ronaldo will play against his former club for the first time since leaving in 2009

Ronaldo atakuwa akicheza dhidi ya timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza tangu aondoke 2009.

No comments:

Post a Comment