KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, February 5, 2013

NEYMAR AWAPONDA ENGLAND AKIDAI WANAMTEGEMEA MTU MMOJA TU AMBAYE NI ROONEY. ASHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA AKIWA ENGLAND, HAPPY BIRTHDAY NEYMAR.

Happy returns: Neymar tweeted this picture of him with birthday cake at Brazil's team hotel today
Neymar alitupia picha hii katika mtandao wa kijamii wa tweeter akiwa hotelini kambini na timu ya taifa ya Brazil.

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil Neymar da Silva Santos JĂșnior 'Neymar' amedai kuwa timu ya taifa ya England haina uzuri wa kuweza kushinda kombe la dunia na kusema kuwa timu hiyo inamtegemea zaidi mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Neymar, ambaye hii leo alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa akifikisha miaka 21 anatarajiwa kupangwa katika mchezo wa kesho wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Simba watatu maalum kwa ajili ya kusheherekea miaka 150 ya chama cha soka nchini England FA.
Amenukuliwa na Sportsmail akisema 
 'England ni timu nzuri na inawachezaji wazuri lakini siwatazami kama wapinzani wetu wazuri katika kombe la dunia.
'Wanawachezaji wazuri wa kufanya vizuri, lakini siwezi kuwalinganisha na Spain na Argentina. 
'Nadhani wanamtegemea sana Wayne Rooney.
Centre of attention: Neymar closes down the ball during Brazil's training session at The Hive in Barnet
Neymar akiwa na kikosi cha Brazil katika mazoezi yaliyofanyika The Hive in Barnet.
Box office: Neymar shares a joke with team-mate Ronaldinho
Ronadinho na Neymar.
Knee-sy does it: Neymar shows off his skills in training
Neymar akionyesha uwezo wa kumiliki mpira.
Listen up: Brazil's coach Luiz Felipe Scolari runs Neymar through his tactics
Luiz Felipe Scolari akimpa maujuzi Neymar.
Ameendelea mshambuliaji huyo akisema,
 'Brazil inawachezaji wengi ambao wanaweza kufunga katika mchezo, kama ilivyo kwa Argentina ambapo kama atakosa kufunga Messi lakini wana Aguero na Tevez, hivyo hivyo kwa Spain kama Iniestia akiwa hayuko katika kiwango kizuri bado wanae Xavi na Villa. Ukirudi kwa Engalnd ukimuweka Rooney huoni mchezaji mwingine anayeweza kufunga'
Neymar amesema Brazil inamatumaini makubwa ya kushinda kombe la dunia nyumbani mwakani.
'Wachezaji wote wanampenda Scolari kama kocha, tunamuheshimu. Ni aina ya mtu ambaye kama unamuheshimu naye anakuheshimu.
'Nadhani alifanya maamuzi sahihi kumrudisha kikosini Ronaldinho. Si tu mchezaji bora katika miaka ya hivi karibuni, lakini ni bora akiwa akiwa uwanjani. Kwa kipindi cha miaka mitatu alikuwa mchezaji bora duniani
London skies: The Samba boys train under the gloomy background of Barnet's training headquarters in Edgware
Timu ya taifa ya Brazil leo imefanya mazoezi huko katika kituo cha mazoezi cha Barnet kitongoji cha Edgware

No comments:

Post a Comment