Hapa wakisubiri treni kwa ajili ya kuelekea London wakitokea Birmingham |
Kuelekea hapo kesho kabla ya mchezo wao dhidi ya timu ya taifa Brazil, wacheaji wa timu ya taifa ya England hii leo walikuwa wakila waki enjoy wakila bata kwa safari ya burudani kuelekea London wakitokea Bimirgham kwa usafiri wa daraja la kwanza.
kikosi hicho cha kocha Roy
Hodgson hapo kesho kitakuwa kikikabiliana na waandaji wa kombe la dunia mwakani Brazil katika dimba la Wembley ambapo leo walisafiri kwa treni kuelekea Birmingham kabla ya kupanda boti kuelekea mji mkuu wa London.
Roy Hodgson (kushoto) akisubiri treni pamoja na wachezaji wake kwenye picha anaonekana Alex Oxlade-Chamberlain
(aliyeshikilia mto) akiongea na Theo Walcott.
Baa ya kuwasili London,
meneja Hodgson akathibitisha kumuanzisha Ashley Cole katika mchezo wa kesho ili akamilishe mchezo wake 100 wa kuitumikia timu ya taifa ya England.
Mlinzi huyo wa pembeni wa Chelsea atakuwa ni mchezaji wa saba wa England kukamilisha idadi hiyo ya michezo ya kuitumikia timu ya taifa maarufu kama simba watatu.
Alipoulizwa kama Cole ataanza, Hodgson aliwaambia waandishi wa habari kuwa
'Ndio ataanza. Ataanza katika mchezo huo, halafu nitaangalia nini cha kufanya kwa Leighton (Baines), ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ashley hakuna shaka ataanza'
Ashley Cole akiongea na nyota wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na Jack Wilshere.
Mchezaji mwingine ambaye bado yuko katika kikosi hicho ni nahodha Steven Gerrard ambaye alikamilisha mchezo wa 100 nevemba mwaka jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Sweden.
Gerrard na Hodgson amekubalina na kupendekeza Cole acheze kesho kukamilisha mchezo wa 100.
Wayne Rooney akiongea na Leon Osman na Leighton Baines
No comments:
Post a Comment