Lionel Messi kwa mara nyingine tena
amefanikiwa kuvunja rekodi nyingine ya dunia kufuatia kufunga bao la 17
katika kila mchezo wa ligi mfululizo akivunja rekodi ilyowekwa katika miaka ya 1930
akiwa na Barcelona.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa
miaka 25 akitokea benchi amefunga bao hilo ambalo limekuwa ni bao lake la 40 tangu kuanza kwa msimu huu bao alilounga
kunako dakika ya 88 ya mchezo na kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa 2-0 dhidi
ya Deportivo La Coruna.
Klabu yake ya Barca imesema Messi ameipita
rekodi iliyowekwa na Pole Teodor Pewterek katika msimu wa mwaka 1937-38 ambaye
alifunga jumla ya mabao 16 katika michezo mfululizo akiwa na Ruch Chorzow.
Hata hivyo
hakuna uthibitisho wa madai ya Barcelona kutoka bodi ya utawala ya shirikisho
la soka duniani fifa juu ya rekodi hiyo.
Messi sasa amefikisha jumla ya mabao
52 katika michezo ya michuano hiyo msimu huu ukijumla na na mabao 5 ya ligi ya
mabingwa.
Desemba ya mwakam jana Messi
alivunja rekodi ya dunia ya kufunga magoli 85 iliyowekwa na Gerd mwaka 1972.
No comments:
Post a Comment