Nigeria itashiriki mataifa ya mataifa ya Afrika 2014 kwa wachezaji wa ndani CHAN baada ya kuamua kutengua maamuzi yao ya
awali ya kujitoa katika michuano hiyo.
NFF ilitangaza mwezi uliopita kuwa haitashirikia kwasababu ya kupunguza gharama.
Sasa taiofa hilo la Afrika magharibi litacheza na Ivory
Coast katikam mchezo wa kufuzu mjini Calabar mwezi June kusaka tiketi ya fainali zake ambazo zitafanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Mazembe yambadilisha kazi aliyekuwa kocha wake Ndiaye kuwa mkurugenzi wa ufundi.
TP Mazembe imemuondoa
kocha wake Lamine Ndiaye kutoka katika kazi yake ya ukocha na kumpeleka katika
nafasi nyingine ya mkurugenzi wa Ufundi.
Kocha huyo wa zamani wa Senegal alitangaza
mwenyewe kuachia ngazi baada ya klabu hiyo ya DR Congo kushindwa kufuzu katika hatua
ya mtoano ya ligi ya mabingwa Afrika na Orlando Pirates ya Afrika kusini
Jumapili.
Hata hivyo mmiliki wa Mazembe Moise Katumbi amekataa
kujiuzulu kwake na sasa amembadilishia majukumu .
Sambamba na kutafuta upya kocha mpya kuziba
nafasi yake Katumbi amesema ana mpango wa kufumua mpya uongozi wa klabu ikiwa
ni pamoja na kutengeneza upya kamati ya habari ya klabu hiyi kufuatia baadhi
yao kusimamishwa.
Benitez: Inahuzunisha kuondoka Chelsea
Rafa Benitez amesema kuwa inahuzunisha
kuondoka na kuiacha Chelsea mwisho wa msimu lakini anataka kuondoka kwa mafanikio.
Benitez ataondoka Stamford Bridge kiangazi
kufuatia kumalizika kwa mpango wa kuongoza klabu hiyo kwa muda ambapo alichukua
mikoba hiyo toka kwa Roberto Di Marteo mwezi November.
"ina huzunisha kiasi unapoondoka lakini
ni sehemu ya kazi yangu,"
"Naona uzoefu ndani ya klabu klabu kuwa
kuna sura chanya. Iko katika nafasi ya juu na kuna wachezaji wazuri iko vizuri"
"Lengo langu ilikuwa ni top four, top
three. Sasa tuko katika fainali ya Europa League na tunajaribu kutaka kushinda
fainali , mambo yako hivyo.
No comments:
Post a Comment