Rais Dilna Roussef wa Brazil ameahidi kusikiliza kilio
cha waandamanaji ambao wameandamana nchi
nzima kupinga gharama kubwa za maandalizi ya
michuano ya kombe la Dunia la kandanda.
Maadamano hayo ni makubwa kabisa kuwahi
kushuhudiwa nchini humo katika kipindi cha zaidi ya
miaka 20. Roussef aliyapongeza maandamano hayo
hapo jana ambapo amesema yameonyesha nguvu
ya demokrasia yao, nguvu ya sauti iliyoko mitaani na
nguvu ya kiraia ya wananchi wao.
Katika hotuba
yake katika Kasri la Rais amesema kwamba sauti
hizo zinapaswa kusikilizwa na kwamba serikali yake
inasikiliza sauti hizo zinazodai mabadiliko.
Leo zaidi ya wananchi 200,000 wa Brazil wameingia
tena barabarani. Maandamano hayo ambayo kwa
kiasi kikubwa yanaongozwa na wanafunzi yalianza
yakiwa madogo na yalichochewa na kupanda kwa
nauli za usafiri wa umma baadaye kupitia mitandao
ya kijamii yaligeuka kuwa vurugu na kulenga
gharama kubwa za maandalizi ya michuano ya
Kombe la Dunia mwaka 2014 na Michuano ya
Olimpiki ya mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment