Wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, hawajapokea
marupurupu yao baada ya kuiwakilisha nchi katika kinyanganyiro cha michuano ya Cosafa
kilichoandaliwa Zambia Julai.
Viungo kadhaa wa timu hiyo ambao waliomba wasitajwe majina yao wameeleza tovuti
hili kwamba tangu kuwasili kutoka shindano hilo, hawajapokea hela zozote
kwa muda waliokuwa wakicheza kama nchi alikwa katika kombe hilo la
mataifa ya Afrika kusini.
“Tunahisi kwamba maafisa wa shirikisho la kandanda wametutenga kwani
hakuna ambaye amefuatilia marupurupu yetu ya Cosafa na tunahofia kuwa
hatutalipwa. Ni muhimu kwa shirikisho kutekeleza matakwa yake,” mchezaji
mmoja aliongeza.
Wakati huo huo, mwenyekiti wa shirikisho, Sam Nyamweya, alikanusha
madai hayo akisema kwamba wachezaji walipaswa kunyakua fedha za
ushindi katika kombe hilo ndio wapate kulipwa.
“Tulituma kikosi chetu katika shindano la Cosafa na makubaliano
kwamba watapigania kitita cha ushindi lakini walikosa kufuzu huku
wakielewa kwamba tulishiriki kwa mwaliko. Tuliwalipa marupurupu yao ya
hapa nyumbani lakini hatuna nia ya kuwakata moyo.
“Tutatafuta fedha na kuona vile tutawalipa lakini wanafaa kuelewa
kuwa jukumu lao lilikua kushinda kombe hilo,”
Harambee Stars waliaga mashindano hayo na kurejea nyumabnai kwa makundi baada ya kupoteza mechi yao ya mwisho dhidi ya Botswana.
No comments:
Post a Comment