KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 7, 2013

CHELSEA WANASEMA DAVID LUIZ HAUZWI.

Chelsea imepokea ombi kutoka katika klabu ya Barcelona la kutaka kumsajili mlinzi wa kimataifa wa Brazil David Luiz.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye alijiunga na Chlesea akitokea katika klabu ya Benfica kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 21 januari 2011 amekuwa katika mawindo ya kigogo hicho cha Katalunya.

Chelsea imeonyesha kusisitiza kuwa Luiz, ambaye amechezea klabu yake michezo zaidi ya 100 hauzwi.

Ombi hilo la Barca linaonekana kuwa ni ombi la pesa taslimu na kwa mpango wa kubadilisha na mchezaji mwingine.

Mkongwe Carles Puyol alikumbwa na matatizo ya mguu msimu uliopita ambapo mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 35 alilazimika kufanyiwa upasuaji wakati ambapo walinzi wengine Gerard Pique, Adriano Correia na Javier Mascherano walikumbwa na majeraha au kusimamishwa.

Mlinzi wa kati wa Paris St-Germain Thiago Silva alikuwa akihusishwa kuelekea Nou Camp lakini Mbrazil huyo alisaini mkataba mwingine wa kuongeza muda wake ndani ya klabu yake mwezi uliopita.

Bayern Munch pia ilikuwa ikihusishwa na kumtaka Luiz, ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano wa kuendela kusalia darajani.

No comments:

Post a Comment