KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 15, 2013

Kocha wa zamani wa Yanga amchefua kocha wa Nigeria Stephen Keshi.

Kocha wa kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi ameonekana kukerwa na ombi la chama cha soka cha Malawi (FAM) la kutaka mchezo baina yao wa kuwani kufuzu fainali ya kombe la dunia ufanyike mwezi ujao.
FAM iliiandikia shirikisho la soka duniani FIFA barua ya kutaka mchezo wa kundi F dhidi ya Super Eagles kuondolewa kutoka katika mji wa Calabar kufuatia hali ya usalama kuwa ya wasiwasi.
Kocha wa timu ya taifa ya Malawi raia wa Belgian Tom Saintfiet amewaambi waandishi wa habari nchini Malawi hajisikii vema mchezo huo kuchezwa katika mji huo kutoka na ukweli kwamba kuna hali ya wasiwasi juu ya usalama.
Hata hivyo kocha wa upande wa pili wa Nigeria Keshi, ambaye kikosi chake kinaoongoza kwa alama mbili juu ya Malawi amesisitiza kuwa uwanja huo hauwezi kubadilishwa
Mamlaka ya soka nchini Nigeria imetoa taarifa kupitia kwa mkuu wa jeshi la poli (Inspector-General of Police) Mohammed Abubakar akisema ameweka na kuimarisha hali ya usalama kwa kiwango cha juu

No comments:

Post a Comment