KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 15, 2013

Moyes kutupa karata ya mwisho kwa Fabregas endapo ataanzia benchi wakati wa michezo ya ligi.

Last ditch: Manchester United will make a final bid for Cesc Fabregas despite him wanting to stay
Manchester United kuweka ofa nyingine ya Cesc Fabregas.
Thumbs up: Moyes has already had two bids rejected for the former Arsenal midfielder
Moyes tayari amesha wasilisha ofa mbili zilizopigwa chini na kiungo wa zamani wa Arsenal Fabregas.

Manchester United itaweka ombi lake la mwisho kwa nguvu zote la kutaka kumsajili Cesc Fabregas kutoka katika klabu ya Barcelona endapo kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania ataona kama atakuwa nje ya kikosi Nou Camp kuelekea kuanza kwa msimi mpya wa ligi.
United iliendelea na ushawishi wake kwa Fabregas mwishoni mwa juma lakini kiingo huyo alisisitiza kupitia mkutano wake na waandishi wa habari kwa kusema anataka kusalia na klabu yake ya sasa.
Kauli ya United ilikuwa ni tunaheshimu maamuzi ya Cesc Fabregas.
'We respect Cesc's decision.'.

Hata hivyo imefahamika kuwa United inaendelea kumfuatilia Fabregas na inafikiria kurejea na ombi la mwisho kwa kuongeza kiasi cha fedha ambacho ni pauni milioni £32 endapo kiungo huyo zamani wa Arsenal ataanza michezo ya msimu mpya wa ligi ya Hispania La Liga akianzia benchi.
Fabregas hatakuwepo katika mchezo wa kwanza wa ligi baina ya Barcelona na Levante Jumapili kufuatia kusumbuliwa na kifundo cha mguu amaumivu aliyoyapata katika mchezo wa maandalizi ya kuanza msimu nchini Malaysia mwishoni mwa juma.
Hata hivyo anatazamiwa kurejea katika hali yake ya kawaida kwa wakati.
Iniesta
Xavi

Fabregas anawasubiri jamaa hapo juu Xavi (kushoto) na Andres Iniesta

Anatarajiwa kuwa salama Jumatano ijayo wakati wa mchezo wa Super Cup dhidi ya Atletico Madrid na kuendelea na michezo mingine ya ligi ya Hispania La Liga kabla wakati huo United itakuwa ikitupia macho kuona kama anacheza au hana nafasi ya kikosi cha kwanza na mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Agosti.
Moja ya sababu inayompa kiburi meneja wa United David Moyes juu ya kumpata Fabregas ni kufuatia kiungo huyo kuonekana kusubiri nje ya uwanja wakati Xavi na Andres Iniesta wakiwa ndio roho ya kiungo cha Barcelona.
United imekwisha kukataliwa ofa zao mbili za awali ikiwepo na rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni £31 wakati mpango huo wa kumnasa Fabregas ulipoanza mwezi uliopita.
Out of action: Fabregas is currently injured with an ankle ligament sprain
Fabregas.

No comments:

Post a Comment