KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 11, 2013

Giovanni Trapattoni nje kuifundisha Ireland baada ya kichapo cha Austria.

Meneja Giovanni Trapattoni ameondoka katika kazi yake ya kuifundisha Jamhuri ya Ireland kufuatia mazungumzo baina yake na chama cha soka cha nchi hiyo baada ya kichapo cha Austria ukiwa ni mchezo wa kuwani kufuzu kombe la dunia.

Chama cha soka cha Ireland kimetangaza kuondoka kwa meneja huyo hii leo baada ya kukutana na Trapattoni na msaidizi wake Marco Tardelli.
Wawili hao walikuwa na mkataba na chama hicho mpaka mwishoni mwa mwezi Mei 2014.
Akiwa kazini kwa miaka miatano, Trapattoni aliiongoza Ireland kufikia fainali ya Euro 2012.

Trapattoni's Ireland record

  • Matches: 64
  • Wins: 26
  • Draws: 22
  • Defeats 16
Kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Austria kumeiiacha Ireland katika hali mbali kimahesabu na kuifanya Sweden kushika nafasi ya pili katika kundi C.

Muda mfupi baada ya mchezo uliopigwa Vienna hapo jana, meneja huyo mwenye umri wa miaka 74 alisikika akisema anasubiri maamuzi ya FAI kuamua juu ya hatma yake ya baadaye.

No comments:

Post a Comment