Klabu ya Al Ahly ya Misri inaingia katika mechi ya mkondo wa pili wa
michuano Klabu Bingwa barani Afrika dhidi Coton Sport ya Cameroon mwishoni mwa wiki
huku ikikabiliwa na matatizo lukuki.
Timu hiyo sasa itabidi kuwa na wachezaji wake
maarufu ambao wamekata tamaa,ikiwa ni pamoja na kutimuliwa kwa kocha na pia kuchezea katika
uwanja usio na mashabiki.
Jambo linaonekana kama ni matukio ya kawaida kwa
timu hiyo yenye rekodi ya kunyakua ubingwa wa Afrika mara saba baada ya
kutoka sare ya 1 -1 nchini Cameroon wiki mbili zilizopita imekuwa
katika hali isiyo ya kuridhisha wiki hii.
Ahly imetoa wachezaji nane wanaochezea timu ya
Taifa ya Misri iliyokubali kipigo cha mabao 6 -1 kutoka kwa Ghana katika
mechi ya mkondo wa kwanza ya kufuzu kucheza kombe la dunia iliyopigwa
siku ya jumanne, na kuondoa matumaini ya Misri kwenda kucheza fainali
hizo nchini Brazil mwaka 2014.
Baada ya kuona ndoto ya kucheza kombe la dunia
imefifia mchezaji mkongwe anacheza nafasi ya kiungo Mohamed Aboutrika
amesema atastaafu soka baada ya michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika
kumalizika.
No comments:
Post a Comment