Meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex
Ferguson amesisitiza kuwa hatarejea katika shughuli za
ukocha wa soka.
Manchester United hivi sasa wanashikilia nafasi
ya 12 katika Ligi Kuu ya England chini ya uongozi wa David Moyes,
aliyeshikilia nafasi hiyo baada ya Ferguson kustaafu mwishoni mwa msimu
uliopita.
"Mimi sina hamu ya kuwa meneja tena ,na
kujisumbua roho yangu ," alisema Ferguson. "United wako mikononi mwa
uongozi mzuri. David atakua poa. Ni meneja mzuri."
Ferguson, mwenye umri wa miaka 71,alidokeza kwamba Roman Abramovich alimtaka aiongoze Chelsea alipoinunua mnamo mwaka 2003.
"walimtuma wakala aniulize Abramovich alipochukua madaraka kwa mara ya kwanza ya klabu hiyo lakini niliwaambia 'Ng'oo."
No comments:
Post a Comment