KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 2, 2013

DROGBA ANASEMA HAKUISHA NA KWAMBA ANADHIHIRISHA HILO KWENYE MICHUANO YA VILABU ULAYA.

 Didier Dragba amesema kuwa uhamisho wake wa mwezi Januari wa kujiunga na Galatasaray ulichagizwa na hamu yake ya kutaka kucheza tena Champions League barani Ulaya.

Mkongwe wa kimataifa wa Ivory Coast aliihama Chelsea na kuelekea Uchina wakati wa kiangazi mwaka jana 2012 baada ya kuisaidia Chelsea kutwaa taji kubwa la vilabu Ulaya mwezi Januari.

Galatasaray ilifika katika hatua ya robo fainali msimu uliopita na Drogba anataka kuonyesha kuwa bado yumo katika kiwango cha juu cha kucheza michuano hiyo.

"Nilipokuwa China nilikuwa ni waza kuwa bado nilikuwa na kitu cha kusema kuhusu soka la Ulaya" Amenukuliwa Drogba mwenye umri wa miaka 35 alipokuwa akiongea na Tuttosport.

"Sikuwa nimekwisha, nilikuwa na nguvu zote na nilitaka kutetea taji nililoshinda nikiwa na Chelsea. Nilidhani kuthibitisha ndani ya Champions League.

"Umri si tatizo bali ni namba. Kila kitu kinategemea ubora wako, uzoefu na afya.

Galatasaray inakibarua pevu dhidi ya Juventus usiku huu.

No comments:

Post a Comment