KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, October 19, 2013

KOCHA WA YANGA BRANDTS ATAMBA KWA KIKOSI IMARA.

Young Africans wamerejea wamerejea jijini Dar es salaam wakitokea kisiwani Pemba ambako walikuwa wameweka kambi ya maandalizi ya mchezo huo.
Kikosi cha Young Africans ambacho kinashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi kikiwa na pointi 15, alama tatu nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Simba SC kitashuka dimbani kesho jumapili kwa lengo la kusaka alama tatu muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo.
Young Africans ambayo inanolewa na kocha mholanzi Ernie Brandts ambaye amekaririwa na mtandao wa klabu hiyo akisema anatambua michezo ya watani wa jadi duniani kote huwa ni migumu lakini kwa sasa haoni sababu itakayowazuia kuibuka na ushindi katika mchezo huo japokuwa Simba timu nzuri pia.
'Ushindi kwetu siku ya jumapili ni muhimu, ni muhimu kwa sababu tunapigania kutetea tena ubingwa wetu kwa awamu ya pili mfululizo, kikubwa tunawaomba wapenzi, washabiki na wanachama waje kwa wingi kuwashangilia vijana wao watakpokuwa wanapeperusha bendera ya watoto wa jangwnai.'

No comments:

Post a Comment