Ross Brawn ataacha kuiongoza timu ya Mercedes ya
mashindano ya magari ya langalanga ya Formula One, kufikia mwisho wa
msimu huu.
Brawn na timu hiyo ya Mercedes wameshindwa
kuafikiana kuhusu wajibu wake katika timu hiyo, kulingana na taarifa za
kuaminika kutoka timu hiyo ya mashindano ya magari.
Timu ya Mercedes sasa itaongozwa na wakurugenzi wawili watakaoshirikiana pamoja, Toto Wolff na Paddy Lowe, na vile vile kutoka kwa Niki Lauda, ambaye ni mwenyekiti mkuu asiyekuwa na mamlaka rasmi ya kufanya uamuzi katika kuiendesha timu hiyo.
Mercedes, na hata Brawn, walikataa kuzungumza kuhusu kinachoendelea kati yao.
Hatua ya kuamua kuondoka kwa Brawn inaafikiwa baada ya miezi mingi ya kushauriana na wakuu wa timu ya Mercedes.
Brawn, ndiye aliyechangia mno katika umaarufu wa
Mjerumani Michael Schumacher kuweza kulinyakua taji la ulimwengu mara
saba katika mashindano ya langalanga, wakati alipokuwa mkuu wa timu za
Benetton na vile vile Ferrari.
Brawn pia alihusika katika ushindi wa Jenson
Button, alipoibuka bingwa wa msimu wa mwaka 2009, na alipojisajili kama
mtu binafsi asiyekuwa na kampuni, kwa jina Brawn GP , kufuatia timu ya
Honda kujiondoa katika mchezo huo.
Hatimaye timu ya Mercedes ilichukua usukani kutoka kwake mwaka 2010
No comments:
Post a Comment