Bingwa wa mchezo wa Kung fu nchini Misri, Mohammed
Youssef amevuliwa medali yake ya dhahabu baada ya kuonesha ishara ya
kumuunga mkono Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi.
Youssef alipigwa picha katika mashindano nchini
Urusi akiwa amevaa T-shirt yenye alama yenye kuonesha ushirikiano na
Waandamanaji wanaomuunga mkono Morsi.
Serikali ya Misri imekuwa ikipambana na waandamanaji tangu baada ya Morsi kuondolewa madarakani mwezi Julai.
Kaka wa mwanamichezo huyo Hammam amesema Youssef
alirudishwa nyumbani kutoka kwenye mashindano hayo na kuhojiwa
alipowasili nchini mwake.
Mkurugenzi wa chama cha Kung Fu nchini Misri,
Gamal El-Jazzar amesema Youssef atafungiwa kuiwakilisha Misti kwenye
michuano ya dunia ya mchezo huo, hata hivyo haijafahamika kama
atafungiwa moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment