KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, October 18, 2013

Pep Guardiola awambia wachezaji wake wamfuate yeye.

Bosi wa Bayern Munich Pep Guardiola amesema wachezaji wake wanapaswa kukubali maamuzi yake endapo mambingwa hao wa Ulaya na Ujerumani watakuwa wanataka kutetea taji lao la Bundasliga msimu huu.
Bayern, ambao walishinda taji ya German Cup na ligi ya mabingwa Ulaya msimu uliopita wanajipanga kuelekea kucheza mchezo wao wa 34 nchini Ujerumani bila kufungwa hapo kesho Jumamosi.
Watakuwa ni wenyeji wa Mainz katika dimba la Allianz Arena.

Ratiba ya michezo ya Kesho Jumamosi


  • Bayern Munich v Mainz (14:30 BST)
  • Borussia Dortmund v Hannover (14:30 BST)
  • Real Madrid v Malaga (15:00)
  • Paris St-Germain v Bastia (16:00)
  • Osasuna v Barcelona (19:00)
Sunday
  • Sochaux v Monaco (13:00)
  • Fiorentina v Juventus (14:00 BST)
  • Torino v Inter Milan (19:45)
Amenukuliwa Guardiola akisema 
"Tutapigania taji la Ujerumani mpaka mwisho wa msimu mchezo lakini endapo kila mchezaji atakubaliana na maamuzi yangu, vinginevyo tutapata matatizo"
Vinara hao wa Bundasliga bado hawajafungwa wakiwa na alama moja tofauti na wanaowafuata Borussia Dortmund wakiwa wanamichezo sita ya ushindi katika michezo yao.
Endapo wataepuka kichapo kutoka kwa Mainz, Bavarians watakuwa na michezo miwili nje ya uwanja wa nyumbani kuelekea kuifikia rekodi ya Hamburg ya kutokupoteza michezo 36 rekodi waliyo iweka mwezi Januari 1983.
.

No comments:

Post a Comment