Gareth Bale, mchezaji aliyeandikisha rekodi ya
kununuliwa kwa bei ya juu zaidi duniani, ni miongoni mwa wachezaji 23
wanaoshindania tuzo ya Fifa ya mchezaji bora zaidi.
Bale, kutoka Wales, na mwenye umri wa miaka 24,
aliifungia Tottenham magoli 26 msimu uliopita, kabla ya kununuliwa na
Real Madrid kwa kitita cha pauni milioni 85.
Kati
ya wachezaji wengine wa ligi kuu ya Premier waliopo katika orodha fupi
ya wachezaji wenye matumaini ya kulinyakua tuzo la Ballon d'Or ni pamoja
na Eden Hazard, Mesut Ozil, Luis Suarez, Yaya Toure na Robin van
Persie.
Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi, pia naye
ana matumaini ya kulipata tuzo hilo, ambalo ameshinda kwa miaka minne
mfululizo iliyopita.
Wachezaji wenzake wenye matumaini ni pamoja na
Andres Iniesta, Neymar, aliyejiunga na timu hiyo ya Nou Camp kutoka
Santos, na vile vile Xavi.
Cristiano Ronaldo wa timu ya Real Madrid pia yumo.
Mshambulizi wa Manchester United, Wayne Rooney, mwaka jana jina lake lilikuwepo katika orodha fupi, lakini mwaka huu halipo.
Bayern Munich ya Ujerumani ambayo iliishinda
Barcelona katika juhudi za kuwa bingwa barani Ulaya, ina majina ya
wachezaji sita katika orodha fupi.
Majina hayo 23 yatapunguzwa hadi majina matatu
mwezi Desemba, kabla ya mshindi kutangazwa mjini Zurich, Uswisi, tarehe
13 mwezi Januari, mwaka 2014.
Kocha wa zamani wa Bayern, Jupp Heynckes, ambaye
wadhifa wake ulichukuliwa na Pep Guardiola, naye ana matumaini ya
kutajwa kama mshindi wa tuzo ya kocha bora zaidi wa mwaka.
Meneja wa zamani wa Manchester United, Sir Alex
Ferguson, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, Jose Mourinho wa Chelsea na
Rafael Benitez wa Napoli, wote watashindania tuzo hiyo ya kocha bora
zaidi, katika orodha ya majina ambayo ina makocha kumi.
No comments:
Post a Comment