Newcastle wakiwa katika uwanja wao nyumbani wa St.
James Park jumamosi hii wameisambaratisha Chelsea kwa jumla ya magoli 2
-0 katika mechi ya ligi kuu ya England.
Newcastle walianza kusherekea ushindi baada ya
kupata goli la kuongoza katika dakika ya 67 lililofungwa kwa kichwa cha
kuchumpa na Yoan Gouffran.
Wakicheza kwa kujiamini Loic Remmy wa Newcastle
alizidi kupigilia mwiba mkali kwa mashabiki wa Chelsea pale alipopachika
goli la pili katika dakika 89.
Kwa matokeo hayo Newcastle sasa itakuwa na point 14 huku na Chelsea ikibakiwa na pointi 20.
No comments:
Post a Comment