KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 1, 2013

CARLO ANCELOTTI AMKOSOA BLATTER KWA SAMAHANI YA KIZUSHI KWA RONALDO.

 Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anadhani msamaha uliombwa na bosi wa shirikisho la soka duniani FIFA kwenda kwa Cristiano Ronaldo haukuwa na ukubwa uliofanana na maumivu ya mchezaji huyo.

Blatter mwenye umri wa miaka 77, hivi karibuni alionyesha mlinganisho wake wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno kwa mshambuliaji mwingine wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi kwa kumfanyia dharau Ronaldo na kuamsha hasira kutoka kwa klabu yake ya Madrid na Ronaldo mwenyewe.

Rais wa Fifa baadaye aliomba radhi kwa maoni yake hayo aliyotoa lakini Ancelotti hajafurahishwa na anaamini bosi huyo mswizz alipaswa kueleweka zaidi.

"Radhi ya Blatter? maumivu yameshafanyika. wakati mwingine unapaswa kufikiri kabla ya kusema kitu. Hata kuhesabu mpaka kumi10,"
 Ancelotti ameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari kabla ya kuelezea kwa kumsafisha na kumpongeza Ronaldo kitabia.

"Cristiano is a very professional and serious player. He gives everything in every game. I can't ask any more from him."
Mtaliano huyo aliendelea mbali zaidi kwa kujadili juu ya kikosi chake cha kwanza kuelekea katika mchezo wa mwisho wa juma dhidi ya Rayo Vallecano na kuweka wazi kuwa atafanya mabadiliko kadhaa kutoka katika kikosi kilichoshinda bao 7-3 dhidi ya Sevilla katikati ya wiki .

"Nitafanya mzunguko kwahiyo wale ambao hawakucheza dhidi ya Sevilla watacheza kesho jumamosi ".

"Raphael Varane anamaumivu kwahiyo hatacheza na anaweza kuwa fiti Jumanne. Xabi Alonso ataanza kesho"

No comments:

Post a Comment