Mshambulizi mahiri wa Barcelona Lionel Messi hauzwi
na kilabu hiyo ambapo klabu hiyo kwasasa inapanga kujadili mkataba mpya na raia huyo wa Argentina,
hii ikiwa ni kauli ya Rais wa kilabu hiyo Josep Maria Bartomeu.
Kumekuwepo na uvumi kuwa Messi ambaye ni mshindi mara nne
wa tuzo la Ballo d'Or, mwenye umri wa miaka 26, analengwa na kilabu ya
Ufaransa ya Pris St-Germain.
Lionel Messi ameisaidia sana Barcelona kufunga zaidi ya mabao 36 katika msimu huu na
amekuwa katika kikosi cha ushindi mara 16 ati ya michezo 20 iliyochezwa.
Katika mahojiano na kituo cha radio cha RAC1,
yaliyonukuliwa katika mtandao wa Barcelona, Bartomeu anasema:
"Kilabu
kitaketi na kushauriana juu ya mkataba mpya. Tutafanya kila tunaloweza
kuhakikisha kuwa yeye ndiye mchezaji anayelipwa mshahara bora zaidi."
Messi alipachika wavuni mabao 60 katika mechi 50
alizoshiriki katika msimu uliopita, na kwa sasa anajitahidi
kufikisha mabao kama hayo msimu huu wa mwaka 2013-14.
Hadi kufikia sasa amefunga mabao 18 na
kati ya hayo ndiyo aliyoyafunga katika Ligi, ingawa amesaidia kufunga
mabao 36 katika mechi 20 alimoshiriki.
No comments:
Post a Comment