Mmiliki wa klabu ya PSG Nasser Al Khelaifi amethibitisha kuwa mabingwa hao wa Ufaransa wanajipanga kumsajili Yohan Cabaye kutoka katika klabu ya Newcastle na kueleza ni kwanini klabu hiyo inahaha kumnasa kiungo huyo.
Taarifa zinaeleza kuwa Cbaye anatarajiwa kukamilisha zoezi la uhamisho huo kwa pauni milioni 20 na kujiunga na PSG hii leo na tayari kiungo huyo ameomba radhi kuwa hatakuwepo katika mchezo wake wa Newcastle dhidi ya Norwich City kwani atakuwa safarini kuelekea Paris kufanya vipimo na kukamilisha mazungumzo ya maslahi binafsi.
Al Khelaifi amemsifu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na kuenda mbali kwa kutoa sababu za kwanini anamtaka Cabaye aelekee Ufaransa.
"tumemchagua Cabaye kwa sababu kuu tatu" alikuwa akiongea na L'Equipe. "moja ni mchezaji mzuri, anatuvutia sana kwa macho yetu.
mbili sijawahi kukutana naye hivi uso kwa macho lakini niliambiwa kuwa ni mtum mzuri pia.
"Three, ni mfaransa ni muhimu kwetu kuchukua wachezaji wa kifaransa kujiunga na PSG, kwa lengo la kuwarejesha katika ligi ya ufaransa"
"Three, ni mfaransa ni muhimu kwetu kuchukua wachezaji wa kifaransa kujiunga na PSG, kwa lengo la kuwarejesha katika ligi ya ufaransa"
No comments:
Post a Comment