Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young
Africans kesho itashuka dimbani kupambana na wenyeji Coastal Union
katika muendelezo wa michezo ya VPL, mchezo utakaopigwa katika daimba la
Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Young Africans ambayo imeshawasili jijini Tanga tangu jana
imefanya mazoezi mepesi asubuhi majira ya saa 2 katika uwanja wa
mkwakwani kujiandaa na mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa Young
Africans kupata ushindi ili iweze kuendelea kukaa kileleni.
Kocha
msaidizi wa Young Africans Charles Mkwasa amesema vijana wake wote fit
kwa sasa baada ya kupata muda mzuri wa kupumzika kufuatia safari ndefu
kutoka nchini Uturuki mwishoni mwa wiki kisha kubadirisha hali ya hewa,
na kwa sasa anasema vijana wako vizuri.
Akiongelea mchezo wa kesho
Mkwasa amesema anajua Coastal Union wana timu nzuri ambayo imekua ikitoa
upinzani mkali kwa timu nyingi za Ligi Kuu lakini anaamini katika
mchezo wa kesho jinsi walivyowaandaa vijana wake watafanya vizuri na
kuwapa furaha washabiki, wapenzi na wanachama wake.
Hali ya kikosi
ni nzuri hata mara baada ya mazoezi ya leo hakuna mchezaji majeruhi
hata mmoja, hivyo wachezaji wote 20 waliokuja jijini Tanga wapo tayari
kwa mchezo huo wa kesho na kazi inabakia kwa benchi la ufundi kuchagua
wamtumie nani katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment