Yohan Cabaye amekamilisha zoezi la vipimo vya afya alivyofanya nchini Ufaransa na anatarajiwa kuwekwa hadaharani kuwa mchezaji rasmi wa Paris Saint-Germain katika mkutano na waandishi wa habari usiku huu.
Newcastle wamekuwa wakisaka mchezaji mbadala yake huku taarifa zikiarifu kuwa tayari wameweka mezani kiasi cha pauni milioni £11 kwa ajili ya kiungo wa Lyon Clement Grenier.
Mpango huo umeaanza asubuhi ya leo huku Cabaye, asubuhi ya leo akionekana kupitia picha mbalimbali akitoka hospitali baada ya kukamilisha vipimo vya afya yake kabla ya kujiunga na PSG kwa uhamisho wa pauni £23.
No comments:
Post a Comment