Inter Milan wako katika mpango wa kumsajili winga wa Manchester United Luis Nani kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu baada ya winga huyo kukubali ofa hiyo kutoka kwa kigogo hicho cha Serie A.
Uhamisho huo unajumuisha juu ya maamuzi mengine ya kumsajili moja kwa moja mwishoni mwa msimu na wanaweza kuelekea mabingwa wa soka wa Premier League United ili kuweza kuwashiwa taa ya kijani.
Uhamisho huo unajumuisha juu ya maamuzi mengine ya kumsajili moja kwa moja mwishoni mwa msimu na wanaweza kuelekea mabingwa wa soka wa Premier League United ili kuweza kuwashiwa taa ya kijani.
Habari za ndani kutoka Nerazzurri zimetanabaisha kuwa mashetani wekundu wanajipanga kuwajibu Inter juu ya ombi lao na kwamba Rais wa Inter Erick Thohir anatarajiwa kufanya kile kinachoelezwa kuwa ni kuweka maandishi rasmi ya kumtaka winga huyo 'rubber stamp the transfer'.
Kocha mkuu wa Inter Walter Mazzarri anatafuta namna ya kuboresha safu yake ya ushambuliaji huku klabu hiyo ikihaha kusaka magoli msimu huu na pia bosi huyu wa zamani wa Napoli ana mtazama winga huyo mwenye umri wa miaka 27 kama ni nyongeza bora katika kikosi chake.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alijikuta katika wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza katika kikosi cha United, akifanikiwa kuanza katika michezo mitano tu chini ya meneja David Moyes.
Nani aliongeza mkataba wake na mabingwa hao wa England mkataba ambao utamuweka na klabu yake hiyo mpaka kiangazi mpaka Juni 2018, lakini kwasasa United wanadhani kuna haja ya kumpunguza winga huyo kwa dhana kuwa kwasasa haitajiki kwa muda huu ingawaje wanataka kumpatia safari ya kucheza kwa muda.
No comments:
Post a Comment