Mwezi mmoja baada ya kujeruhiwa katika ajali ya
mchezo wa kuteleza kwenye barafu, meneja wa jogoo wa mashindano ya mbio
za magari ya langalanga, mjerumani Michael Schumacher amesema
kwamba madaktari wanaendelea kumweka katika hali ya 'kuzirai
kimatibabu', na kwamba yuko katika hali imara.
Bingwa huyo mara saba aligonga kichwa chake
dhidi ya mwamba wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps
nchini Ufaransa.
Madaktari wanatumia madawa kumpa usingizi wakijaribu kupunguza uvimbe na kuchubuka kwenye ubongo wake.
Tayari wametekeleza upasuaji mara mbili kuondoa damu iliyoganda kwenye ubongo.
Hata hivyo huenda maisha yake yakawa hatarini
iwamo ataendelea kuwa katika hali ya kuzirai kutokana na hatari ya
ubongo wake kuharibika na kupata maambukizi ya kifua.
No comments:
Post a Comment