Magoli matatu ya Sergio Aguero na moja la Kolarov kwenye uwanja wa Etihad, yameisaidia Manchester City kuvuka raundi ya nne ya michuano ya kombe la FA.
Shuti dogo la Fernando Forestieri lililozaa goli
na lile la Troy Deeney yaliifanya Watford kuongoza hadi kipindi cha
kwanza kinamalizika katika matokeo ambayo hayakutarajiwa na wengi katika
mechi hiyo ambayo City walipanga kikosi mchanganyiko.
Ilikuwa ni mechi ambayo iliwachukua
Man City saa moja kuweza kuziona nyavu za uwanja wao wa nyumbani pale
Aguero alipomalizia krosi ya Aleksandar Kolarov.
Baadaye Aleksandar Kolarov tena aliachia shuti
kali ambalo lilimshinda kipa wa Watford Jonathan Bond kabla ya Aguero
hajautumbukiza mpira wavuni na kufanya matokeo kuwa 2-2 dakika ya 79.
Wakati Watford wakijuliza namna ya kurejesha
mabao hayo Aleksandar Kolarov aliifungia bao la tatu Man City kwa shuti
kali nje ya eneo la hatari na kuweka matumaini ya miamba hiyo ya
Kaskazini mwa kisiwa cha England kuuendelea na mbio zao za kunyakuwa
taji la FA msimu huu.
Ni Aguero kwa mara nyingine aliyeibuka shujaa wa
mchezo kwa Man City baada ya kupiga kichwa mpira uliomkuta upande wa
kushoto wa eneo la ndani ya kumi na nane,krosi pasi nzuri kutoka kwa
Jesus Navas.
Liverpool waliifunga Bournemouth kwa mabao mawili kwa bila, mabao ya Victor Moses na Daniel Sturridge.
Katika mchezo huo, kocha wa Liverpool Brendan
Rogers alishusha kikosi kamili cha majogoo wa Anfield katika mchezo huo
wa ugenini.
Katika michezo mingine, Birmingham ilikubali kichapo cha mabao1-2 kutoka kwa Swansea.
Bolton wao wakiwa nyumbani walilala kwa 0-1
dhidi ya Cardiff bao likifungwa na Fraizer Campbell kinda la zamani wa
Manchester United.
Huddersfield ikafungwa 0-1 na Charlton.
Port Vale yenyewe ililala 1-3 mbele ya Brighton.
Rochdale ikafungwa na Sheff Wed1 - 2 katika mchezo uliokuwa mgumu.
Southampton imeifunga Yeovil 2-0 na kujihakikishia tiketi ya kucheza raundi ya tano ya michuano ya kombe hilo la FA.
Southend timu kutoka maeneo ya karibu na pwani ya England yenyewe ilikubali kichapo cha 0-2 kutoka kwa Hull.
Wakati Sunderland ambao wamekwishajikatia tiketi
ya kucheza fainal ya kombe la ligi baada ya kuitoa Manchester United
kwenye nusu fainal, wao waliichapa Kidderminster 1-0 kwenye uwanja wa
Stadium of Light.
Wigan timu iliyoshuka daraja msimu uliopita
yenyewe ilionyesha makali yake na nia yao ya kurejea ligi kuu kwa
kuitandika Crystal Palace 2-1.
NA Everton wakiwa ugenini waliiadhibu Stevenage kwa kuichapa mabao 4-0 kwenye uliokuwa mwepesi kwa kikosi cha Roberto Martnez.
No comments:
Post a Comment