Madirisha haya mawili pichani ni baada ya kuvunjwa kwa vitofa katika basi la mashabiki wa Hull City. |
Shabiki wa klabu ya Hull City amelazimika kukimbizwa hospitali kufuatia basi la mashabiki wa klabu hiyo kuvamiwa karibu na uwanja wa Anfield baada ya kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Liverpool siku ya mwaka mpya.
Tofari lilirushwa dirishani ambapo mashabiki wa Hull City walikuwa wamedhamiriwa na wavamizi hao kutokana na kukasirishwa na mashabiki hao.
Peter
Shipp, mwenyekiti wa kampuni ya mabasi ya 'East Yorkshire Motor Company amenukuliwa akisema
'Lilikuwa ni basi la mwisho kuondoka katika msafara na nadhani tukio hilo limetokea takribani dakika tano mpaka kumi baada ya kuondoka Anfield.
Lazima watakuwa ni 'mindless idiots fulani hivi'. Kitofa likirushwa kuelekea dirishani na kumpiga dereva. Kwa bahati hakuumia.
Picha ikionyesha uharibifu baada ya tukio la kurushwa kitofa dirishani.
'Abiria wawili au watatu walishuka kukabiliana na wahuni hao na mmoja alipigwa na tofali mgongoni. Kwasasa yuko hospitali. Hakutaka kwenda hospitali lakini asubuhi hii ameelekea huko'.
Dereva wa basi hilo alifanikiwa kulipeleka basi hilo katika kituo cha karibu cha mabasi na kutuma gari lingine kuwachukua abiria wengine kwenda Hull.
Polisi wa kitongoji cha Merseyside wanachunguza tukio hilo ambalo limetokea Townsend Avenue, karibu na Anfield, takribani saa 5.35pm.
Maafisa wanafuatilia kupitia mitambo ya CCTV na kuongea na kampuni ya mabasi hayo na mashahidi wengine kuanzia katika eneo hilo kujua kilichotokea na kuwanasa waliohusika.
Ujumbe wa mtandao wa twitter kutoka 'Hull City 'Ulltras', ambaye alikuwepo katika basi wakati wakivamiwa.
No comments:
Post a Comment