Hatimaye Cardiff City imekamilisha mipango ya kumuuajiri Ole Gunnar Solskjaer kuwa meneja mpya wa klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United hii leo amekutana na kikosi chake katika uwanja w mazoezi asubuhi ya leo na ataanza kuitumikia klabu hiyo akiwa kazini katika mchezo dhidi ya Newcastle United mchezo wa michuano ya FA Jumamosi.
Solskjaer anajiunga na klabu hiyi akitokea katika klabu ya Molde FK ya nchini Norwey na atakawa akichukua nafasi ya Malky Mackay aliyefutwa kazi baada ya na mmiliki wa klabu hiyo Vincent Tan mwezi uliopita.
Akikaririwa meneja huyo mpya amesema
‘It is a fantastic challenge, Cardiff iko tayari kuelekea katika hatua ya mbele zaidi. Nina matumaini nitaisaidia.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 40 kwasasa alikuwa Emirates Stadium jana wakati wa mchezo ambao Bluebirds walifungwa na Arsenal na ameahidiwa fedha nyingi kwa ajili ya kufanya usajili wa dirisha ndogo ndani ya mwezi huu wa Januari.
Solskjaer, ambaye alikuwepo katika kikosi kilichoshinda Champions League dhidi ya Bayern Munich mwaka 1999, ambapo pia aliichezea United jumla ya michezo 235 na kushinda mataji sita ya ligi kuu ya soka nchini England 'Premier League' pamoja na michuano ya FA akiwa na klabu hiyo yenye maskani yake Old
Trafford.\
Baada ya kustaafu kucheza soka mwaka 2007, Solskjaer alikuwa katika kikosi cha pili cha United 'reserve
team' kwa miaka miwili na nusu kabla ya kuiongoza Molde iliyoshinda taji la ligi kuu ya soka Norwey mwaka 2011.
Historia ya makocha raia wa Norwey ni mbovu nchini England
Ni mwingereza mmoja tu katika historia ya soka la Norway ambaye aliwahi kufundisha soka katika vilabu vinavyoshiriki ligi ya Premier League ambaye hata hivyo hakumaliza kwa mafanikio.
Egil Olsen alikuwa meneja wa Wimbledon mwaka 1999 lakini alimaliza kwa kipindi cha pungufu ya nusu msimu ambapo Dons iliteremka daraja kutoka Premiership
(Takwimu za kushuka kwa Dons katika michezo yote ilikuwa kama inavyoonekana hapo chini)
Games | Won | Drew | Lost | For | Against | Win% |
---|---|---|---|---|---|---|
43 | 11 | 12 | 20 | 55 | 80 | 25.58 |
Wengine kutoka Norway waliowahi kufundisha soka England ni katika ligi ndogo ya Championship. Henning Berg aliwahi kuwa meneja wa Blackburn kwa kipindi cha siku 57,
aliandikisha ushindi katika mchezo mmoja, sare tatu na kuchapwa michezo sita katika kupindi chake na kuondolewa kazini.
Stale Solbakken
alikua tatizo katika klabu ya Wolves katika nusu ya kwanza ya msimu uliopita, ambapo aliaanza kampeni na kumaliza kwa kushuka mpaka League One.
Takwimu za Wolves.
Games | Won | Drew | Lost | Win% |
---|---|---|---|---|
30 | 10 | 5 | 15 | 33.33 |
No comments:
Post a Comment