Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amewashutumu West Ham United kwa
kucheza "soka ya karne ya kumi na tisa” baada yao kunusuru sare ya 0-0
dhidi ya timu yake.
Chelsea walitawala mechi hiyo iliyochezewa Stamford Bridge jana Jumanne,
lakini wakashindwa kupenya ukuta uliowekwa na vijana hao wa Sam
Allarydce.
Hii ina maana kwamba walikosa fursa ya kupanda hadi nambari ya pili
katika msimamo wa ligi, na kuwaachwa kwa alama tatu nyuma ya viongozi wapya
Manchester City, ambao watakutana nao Jumatatu uwanjani Etihad.
"Ni vigumu sana kucheza mechi ambapo ni timu moja pekee inataka
kucheza,” alisema Mourinho. "Vigumu sana. Mechi ni ya timu mbili. Katika
mechi hii, ni timu moja pekee iliyokuwa ikicheza, na hiyo nyingine
haikuwa ikicheza.
“Nilimwambia Big Sam (Allardyce), na narudia maneno yangu, kwamba
wanahitaji alama. Kwa sababu wanahitaji alama, kuja hapa na kutocheza na
kufanya walivyofanya, hili halikubaliki? Labda ndio.
“Siwezi kuwakashifu sana kwa sababu ningekuwa katika hali sawa, sijui
kama labda naweza kufanya tu vile. Labda naweza kufanya hivyo. Kwa
hivyo, siwakashifu kwa hilo.
“Lakini, hii si Ligi ya Premia. Hii si ligi bora zaidi duniani. Hii ni soka ya karne ya kumi na tisa. Ni hali ya kusikitisha.”
Alipoulizwa alikuwa anamaanisha nini akisema ‘soka ya karne ya kumi
na tisa’, Mourinho alisema: "Kujifanya kwamba umeumia, kudanganya. Sijui
kama hilo ndilo neno sahihi. Kipa wao kupoteza muda kuanzia dakika ya
kwanza badala ya kusubiri angalao dakika ya 70.
"Madifenda kwenye eneo la hatari, madifenda ambao hawakukanyaga nje
ya eneo la hatari. Mpira wa kipuuzi. Lakini mimi ni nani niwakosoe.Wana
furaha. Walipata alama moja.”
Allardyce alimcheka Mourinho na kupuuzilia mbali ukosoaji wake baada
ya matokeo hayo ambayo yaliacha timu yake ikiwa alama mbili kutoka eneo
la kushushwa ngazi.
"Jose hawezi kukubali hayo, anaweza?" meneja huyo wa West Ham
alisema. "Hawezi kwa sababu tulimzidi ujanja, tulimuweza. Hawezi
kukubali hayo. Anaweza kuniambia yote anayotaka. Sijali, kusema kweli.
“Ninafurahi kuona wachezaji wa Chelsea wakilia na kusihi refa,
wakijaribu kumshinikiza, Jose akiruka juu chini eneo lake la kiufundi.
Ni jambo zuri sana kutazama.”
Mourinho alikataa kukosoa timu yake, na badala yake akasisitiza kwamba walifanya kila waliloweza kushinda.
“Kwa wachezaji wangu, nina furaha,” alisema. “Kipindi cha pili
kilikuwa kikuu. Ulijaribu, tukaunda nafasi, tukashindwa kufunga, kipa
akaokoa, madifenda wakaokoa mawili. Siwezi kulalamika kuhusu watu wangu,
na mimi sina haki ya kukashifu walivyofanya.”
Meneja huyo wa Chelsea alikiri kwamba ushindi wa Manchester City wa
5-1 dhidi ya Tottenham Hotspur ulithibitisha kwamba timu hiyo ya Manuel
Pellegrini huenda ikashinda taji – na hata kushinda timu yake kwa
urahisi wiki ijayo.
“Nimesema jambo hili miezi mingapi? Timu moja (City) ndiyo
iliyokamilika. Hiyo ni nyingine ni timu inayojaribu kujijenga,” akasema
Mourinho.
“Kwangu, hilo halinishangazi. Tutaenda kwao Jumatatu ijayo na
matokeo kwa sasa ni 0-0. Wanapigiwa upatu kushindwa? Ndio. Wanapigiwa
upatu kufunga tena mabao manne, matano, sita? Ndio. Lakini kwa sasa ni
0-0 na tutaenda huko kushindana.”
Allardyce alifurahishwa na alama moja waliyopata, lakini akakiri
kwamba majeraha waliyopata Mohamed Diame na Joey O'Brien yalikuwa
yametia ila kiasi ufanisi huo.
O'Brien alijeruhiwa bega lake mechi ikikaribia kuisha, huku Diame akijeruhiwa goti baada ya kuangukia bango la matangazo.
“Majeraha hayo ni tatizo – Mo alipoangukia bango la matangazo, na Joey akateguka bega,” Allardyce alisema.
"Huko ni kuteguka kwa tatu msimu huu. Sijawahi kuwa na wachezaji
watatu walioteguka msimu mmoja maisha yangu ya ukufunzi. Lakini tuna
wachezaji kadha wanaorudi, ambao wanaweza kuingia kwenye benchi, na
hivyo kikosi ni thabiti na kinaweza kukabiliana na hali.
"Diame amekwaruzwa kwenye goti. Joey atakaa nje wiki10-12."
No comments:
Post a Comment