Juninho Pernambucano ametangaza kustaafu soka la kulipwa atakapo fikisha umri wa miaka 39.
Roberto Dinamite, Rais wa klabu anayochezea Juninho kwa sasa ya Vasco De Gama amesema hilo kwa wanahabari baada ya kikosi cha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Audax.
"Nataka niweke wazi maamuzi ya Juninho Pernambucano rasmi. wiki hii tulizungumza hili na ameamua kuachana na soka ” amesema Dinamite.
Jumatatu, Juninho anatarajiwa kukutana na waandishi wa habari na atakuwa akipokea maswali mengi kutoka kwao.
Kiungo huyo mchezeshaji alijiunga na Vasco mwezi Julai akitokea New York Red Bulls, na hiyo kuwa ni mara yake ya tatu katika klabu hiyo.

Juninho amekuwa dimbani kama mchezaji wa kulipwa miaka 20 iliyopita akianzia katika klabu ya Sport Recife mwaka 1993.
Juninho alielekea Ulaya na kujiunga na Lyon mwaka 2001. aliitumikia kwa kipindi cha nane ndani ya klabu hiyo akishinda mataji saba ya Ligue 1 na alikuwa nahodha wa klabu hiyo baadaye.
Amecheza soka huko na Marekani ya Kaskazini kabla ya kurejea Brazil.
No comments:
Post a Comment