Nyota wa Everton Johnny Heitinga anajipanga kujiunga na Galatasaray baadaya ya bosi Roberto Martinez kutanabaisha kuwa mlinzi huyo amekuwa katika mazungumzo na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki na wakiwa ni mabingwa watetezi wa taji la ligi hiyo.
Heitinga amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Goodison Park kwa karibu mwezi mzima akiwa ameichezea klabu hiyo michezo mitano tangu kuanza kwa msimu.
Wakati dirisha likielekea kufungwa usiku wa kesho inavyoonekana ni kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka atakuwa anaelekea kujiunga na kikosi cha Roberto Mancini.
No comments:
Post a Comment