Kiungo wa Mali Seydou Keita amejiunga na Valencia mpaka kumalizika kwa msimu, taarifa hizi zimethibitishwa na klabu hiyo ya nchini Hispania.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona mwenye umri wa miaka 34 anajiunga na klabu hiyo kwa ada huru akitokea katika klabu ya nchini China ya Dalian Aerbin.
Valencia imesema kupitia katika mtandao rasmi wa klabu hiyo kuwa Keita ataitumikia klabu hiyo mpaka mwezi juni kwa makubaliano ya kuwepo uwezekano wa kumuongezea mkataba.
Keita ameshinda mataji 14 katika kipindi cha misimu minne akiwa na Barcelona
kati ya mwaka 2008 na 2012 na akiichezea nchi yake jumla ya michezo 88 na kufunga magoli 24.
No comments:
Post a Comment