West Ham imemsajili kiungo wa zamani wa Manchester City Abdul Razak kwa mkataba wa muda mfupi akitokea katika klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.
Razak mwenye umri wa miaka 21, ambaye amecheza michezo mitano katika timu ya taifa ya Ivory Coast, alianza kucheza soka katika klabu ya Crystal Palace kabla ya kujiunga na City.
Lakini hakuweza kucheza katika Premier League na amekuwepo kwa kipindi cha mkopo katika klabu mbalimbali za Portsmouth, Brighton, Charlton na Anzhi.
Usajili huu unakuwa ni wa nne kwa meneja Sam Allardyce katika usajili wa mwezi Januari.
No comments:
Post a Comment