Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaingia raundi ya 16 wikiendi
hii kwa mechi nne ambapo kesho (Februari 1 mwaka huu) Simba itakuwa mwenyeji wa
Oljoro JKT katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Oljoro watakuwa wakiingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kibano cha bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Shekh Amri Abedi Kaluta mkoani Arusha.
Bila shaka kocha wa sasa wa timu hiyo Hemed Morocco atataka kurekebisha kusawazisha makosa ya mchezo wa kwanza licha ya mwamba hakuwa na kikosi hicho, huku dhamana ya kusimamia sheria uwanjani akiwa amekabidhiwa mwamuzi Nathan Lazaro kutoka mkoani
Kilimanjaro wakati Kamishna ni Hakim Byemba wa Dodoma.
Uwanja
wa Azam uliopo Mbagala kutakuwa na mchezo mwingine ambapo wenyeji Ashanti
United ya Ilala watakuwa wakikamata vilivyo dhidi ya Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga.
Ashanti watakuwa wakiingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 na Mgambo katika mchezo wa kwanza hivyo ambao ndio ushindi pekee waliowahi kupata Mgambo tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi. Hiyo inamaanisha kuwa Ashanti ndio kibonde pekee cha Mgambo katika ligi hii inayoendelea kwani Mgambo imefungwa mechi kumi na kwenda sare mechi tatu na kushinda mchezo mmoja dhidi ya Ashanti.
Kwasasa Ashanti inanolewa na kocha na mchezaji wa zamani Simba Abdalah Kibadeni ambaye amefanya usajili mzuri kwa kuwaongeza nyota kadhaa ambao wachunguzi wa mambo ya kisoka wamekubali usajili huo ambao umeleta mabadiliko.
Wachezaji hao ni Kassim
Kilungo, Mohamed Banka, Bright Obinna, Victor Costa, Juma Mpongo, Juma
Jabu, Ally Kondo, Shafii Rajab, Mohamed Faki, Abubakar Mtiro, Patrick
Mhagama, Ally Kabunda, Hassan Kabunda, Idd Ally na Rahim Abdallah.
Bila shaka King atahitaji matokeo mazuri katika mchezo huo.
Jumapili
(Februari 2 mwaka huu) ni Yanga vs Mbeya City (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
saa 10 kamili jioni).
Huu ni mchezo ambao unarudisha nyuma kumbukumbu ya matokeo ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mkoani Mbeya matokeo ambayo haikutarajiwa kwa Yanga.
Mbali na matokeo ya uwanjani itakumbukwa kuwa ilitoke vurugu kubwa mara baada ya mchezo huo kiasi klabu ya Yanga kulazimika kukata rufaa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) ikitaka mchezo wake dhidi ya Mbeya City urudiwe katika Uwanja usiofungamana na timu yoyote baina yao.
Yanga kupitia kwa
Mjumbe
wa Sekretarieti yao Mkenya Patrick Naggi wakati huo waliwaambia waandishi wa habari kuwa katika mchezo huo walicheza chini ya kinga (Under
Protest)
Mazingira hayo yanaashiria wazi kuwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu na wa kusisimua, huku pia Mbeya City ambayo haijapoteza mchezo tangu kuanza kwa ligi hiyo, watataka kulinda rekodi hiyo ya UNBEATEN mpaka sasa nao Yanga ambao waliopokonywa usukani wa ligi hiyo na Azam kufuatia sare yao dhidi ya Coastal Union ya Tanga uwanja wa Mkwakwani katikati ya juma, wakihitaji kurejea kwa ushindi wa michezo mfululizo na wakianza na mchezo wa kesho kutwa uwanja wa taifa.
Mbeya City wana kumbukumbu ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo uliopigwa uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani Jumatano.
Kule Chamazi Jumapili ni mchezo mwingine wa ligi hiyo baina ya vinara wa ligi Azam fc dhidi ya Kagera Sugar.
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Februari 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania
Prisons vs Coastal Union (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu
Shooting (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi, Tabora), na JKT Ruvu vs Ashanti United (Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi).
No comments:
Post a Comment